TIRA yatoa maelekezo kuepuka udanganyifu

DAR ES SALAAM :Wamiliki wa kampuni za bima, watu wa wanaohusika na gereji za magari, wametakiwa kufuata mwongozo sahihi wa utoaji wa huduma hizo uliotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Ili kuondokana na malalamiko ya udanganyifu, ucheleweshaji wa malipo na huduma mbovu kwa wateja wao.

Hayo yamesemwa leo Dar es salaam na Kamishina wa Bima Dk Baghayo Saqware katika mwendelezo wa semina kwa watumishi mbalimbali wa huduma za bima nchini, ambapo leo mamlaka hiyo imekutana na kampuni za Bima na Umoja wa Watengenezaji na Warekebishaji wa vyombo vya moto (gereji).

Mwenyekiti wa muda wa Chama Cha Wamiliki wa Gereji, Hendry Lema, ameiomba TIRA kuweka mazingira rafiki ya usajili na kutoa elimu ili kuwafikia watu wengi zaidi, huku wakipendekeza kuwepo adhabu kwa wamiliki wa gereji ambao watashindwa kujisajili na kwamba wakisajiliwa wanaomba waweze kufanya kazi na kampuni zote za bima.

Meneja Madai kutoka Kampuni ya Bima ya Britam, Neema Mathayo akizungumza kwa niaba ya kampuni nyingine ya bima, amesema mwongozo huo unatasaidia kumaliza udanganyifu ambao umekuwa ukijitokeza mara Kwa mara katika huduma zao, huku mwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Lugano Mwasomola akisema mwongozo huo utakuwa na msaada mkubwa.

Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki, Zacharia Muyengi amesema mafunzo hayo ni mwendelezo, ambapo pia washiriki wanafundishwa mifumo ya mamlaka na mfumo wa kujisajili, utaratibu wa nyaraka zinazohitajika wakati wa usajili.

Habari Zifananazo

Back to top button