WACHEZAJI tisa wa Liverpool wataukosa mchezo wa EPL dhidi ya Burnley utakaopigwa uwanja wa Anfiled leo jioni.
Mohamed Salah: Salah: Hajaonekana uwanjani tangu siku ya mwaka mpya kutokana na majukumu yake katika Kombe la Mataifa ya Afrika akiwa na Misri na kuumia wakati akiitumikia Misri. Wakati juhudi za matibabu yake zikiendelea leo pia atakosekana.
Dominik Szoboszlai: Szoboszlai amekuwa akikabiliwa na jeraha la msuli wa paja kwa muda mrefu. Licha ya kurudi kwa muda mfupi dhidi ya Chelsea wiki iliyopita, suala hilohilo la utimamu wa mwili lilimlazimu kukaa nje katika kichapo cha Arsenal na pia ataukosa mchezo wa leo.
Conor Bradley: Bradley hatakuwepo kwenye mchezo wa leo kwani ana majonzi ya kufiwa na baba yake. Babake, Joe Bradley, aliaga dunia siku chache zilizopita, na kupelekea kukosa mechi ya Arsenal.
Thiago Alcântara:Baada ya kurejea na kucheza kwa dakika kadhaa dhidi ya Arsenal, , Thiago alipata jeraha la misuli ya paja wakati wa mechi hiyo. Tarehe yake ya kurudi bado haijafahamika kwani anajiunga na orodha ya waliojeruhiwa kwa mara nyingine tena.
Kostas Tsimikas: Tsimikas amekuwa nje ya uwanja tangu Desemba 23 kutokana na kuvunjika mfupa wa shingo aliyopata wakati wa mechi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Anfield. Ingawa amekuwa akiimarisha mchakato wake wa kupona katika wiki za hivi karibuni, hatarajiwi kujiunga tena na kikosi kwa sasa.
Joël Matip: Jeraha la Matip la ACL linamaanisha kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia. Huku mkataba wake ukimalizika mwishoni mwa msimu huu, inazua maswali kuhusu iwapo ameichezea Liverpool mechi yake ya mwisho.
Ibrahima Konaté: Kufungiwa kwa Konaté mechi moja kutokana na kadi zake mbili za njano kwenye kipigo cha Arsenal kunamhakikishia kutokuwepo kwenye mchezo wa leo wa Burnley.
Klopp hakufurahishwa na uamuzi huo kutoka kwa Anthony Taylor lakini kwa sababu ilikuwa ni kadi mbili za njano, Liverpool hawakuweza kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Stefan Bajčetić:Bajčetić amekuwa nje kutokana na jeraha la mguu na hajashiriki mechi yoyote tangu Septemba. Haijulikani ni lini atakuwa fiti kurejea kikosini.
Mchezaji mwingine ni Wataru Endō ambaye amekosekana katika mechi saba zilizopita za Liverpool kutokana na ushiriki wake katika Kombe la Asia.