TNGP yawataka wanawake kushiriki uchaguzi mitaa

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoka wito kwa waandishi wa habari kuandika habari za kuhamasisha wanawake kushiriki na kijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 2024.

Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, Ofisa Habari wa Mtandao huo, Monica John amesema bado wanawake wamekuwa nyuma kijitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa waandishi kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es salam.

Advertisement

Amesema vyombo vya habari pamoja na waandishi wana wajibu wa kuhamasisha wanawake kushiriki  chaguzi kutokana na tafiti mbalimbali kuonyesha bado wanawake hawashiriki kikamilifu jambo ambalo halileti mgawanyo mzuri wa jinsia katika uongozi.

“Ripoti ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 kutoka ofisi ya Rais- Tamisemi, kwa upande wa vijiji kati ya nafasi 11,915 za wenyeviti wa vijiji wanawake walishinda nafasi 528 ambazo ni sawa na asilimia 2.1 ya wenyeviti wote  huku wanaume ikiwa ni asili 97.9 hivyo bado jitihada zinahitajika,”amesema.

Amesema kuna uhitaji mkubwa wa kushirikishana na kuhamasisha wanawake wengi kugombea jambo ambalo idadi hiyo iliongeza uwezekanao wa kutafuta changamoto zinazowakabili wanawake zitatafutiwa ufumbuzi zaidi.