‘Toeni mapendekezo kutatua changamoto ya ajira’

SERIKALI kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia inaendelea kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wenye thamani ya Dola za marekani milioni 42.50 sawa na shilingi Bilioni 97 ambazo zimetolewa na Benki ya Dunia kwa masharti nafuu.
Lengo la mradi huo ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuboresha mitaala ya programu za kipaumbhele ilikuendana na mahitaji ya soko.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Kamati ya ushauri chuo kikuu cha Ardhi, Katibu Mkuu kiongozi, Dk Moses Kusiluka ameiagiza kamati ya hiyo kuhakikisha wanatoa mapendekezo yatakayosaidia kutatua changamoto ya ajira na kutoa ushauri mahitaji yanayoitajika katika sekta ya ardhi hapa nchini.
Amesema lengo la kuzindua kamati hiyo ni kuboresha mitaala iliyopo kwenye vyuo, ili iweze kuendana na soko la ajira na kuimarisha na kuongeza kuwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kutasaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira hapa nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya hiyo, Prof. Carolyne Nombo amesema uzinduzi wa kamati hiyo utasaidia kuboresha uwezo wa vyuo kuandaa mitaala, kufanya tafiti na kutoa huduma za jamii zinazoendana na mahitaji ya soko.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Ally Namangaya ameahidi kuipa ushirikiano kamati hiyo katika majukumu yake.