MIAMBA ya soka nchini, klabu ya Yanga leo imeikanda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mabao 3-1 katika mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam yamefungwa na Clement Mzize aliyetupia mawili dakika za 33 na 60 huku la tatau likifungwa na Stephanie Aziz Ki dakika 56.
Bao la Mazembe limefungwa kwa mkwaju wa penalti na golikipa Alioune Faty dakika 16.
Yanga sasa inashika nafasi ya tatu kundi A ikiwa na pointi nne baada ya michezo minne wakati TP Mazembe ni mwisho katika msimamo ikiwa na pointi 2.
Al Hilal Omdurman inaongoza kundi ikiwa na pointi tisa baada ya michezo mitatu huku nafasi ya pili ikishikiwa na MC Alger yenye pointi 4.
Timu hizo zitakutana Januari 5.