TPA yakamilisha maboresho Bandari ya Kigoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imesema maboresho yanayofanywa katika bandari za Ziwa Tanganyika ikiwemo Bandari ya Kigoma yanalenga kukidhi mahiti ya wateja wanaotaka kusafirisha shehena kubwa ya bidhaa Kutoka Tanzania kwenda  nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula amesema hayo wakati akifunga Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo mamlaka hiyo ofisi ya Kigoma iliandaa chakula cha jioni kwa wateja wake.

Edward Mabula Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika

Amesema tangu mwaka 2018 uboreshaji ulianza katika Bandari za Ziwa Tanganyika ambapo kiasi cha Sh bilioni 108 kilitumika ikiwa ni sehemu ya mpango wa TPA kuboresha Bandari za Ziwa Tanganyika.

SOMA: Tozo matumizi miundombinu bandari kurudi TPA

Sambamba na hilo amesema kuwa mwaka jana Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) lilitenga kiasi cha Sh bilioni 2 kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Kigoma mpango ulioanza mwaka jana na serikali kupitia (TPA) imeongeza fedha zaidi ambapo mpango huo utakamilika mwakani.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Edward Mabula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wateja wanaotoa huduma katika Bandari ya Kigoma shehena zinazoenda nchi za maziwa makuu

Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo wanaotoa huduma katika Bandari ya Kigoma akiwemo Mbaraka Amour Saidi Mkurugenzi wa Falcon Marine ambao ni wakala wa meli katika Ziwa Tanganyika amesema kuwa maboresho makubwa yanayotakiwa kufanya kwa sasa ni kuboresha zana za kupakia na kupakua shehena.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya shegema ambao ni  Wakala wa Huduma za Meli katika Bandari ya Kigoma, Juliana Mutabiirwa amesema kuwa kazi zinafanyika vizuri tatizo ni vifaa vya kushushia na kupandisha shehena bado yanahitajika maboresho kutokana na mizigo mizito kupitishwa bandari hapo ambayo winchi zilizopo bandari hapo zinazidiwa uwezo.

Mbaraka Amour Saidi Mkurugenzi wa Falcon Marine ambao ni Wakala wa Meli katika Ziwa Tanganyika

Habari Zifananazo

Back to top button