TPSA sasa kwenda kimataifa

DAR-ES-SALAAM: Chama cha Kuogelea kwa watu wenye ulemavu (TPSA) kimepata uanachama wa muda wa Shirikisho la Kimataifa la Michezo kwa watu wenye ulemavu wa kiakili (Virtus).

Akizungumza na SpotiLeo Katibu Mkuu wa TPSA Ramadhan Namkoveka amesema uanachama huo ni wa muda wakati wakielekea kupata uanachama kamili itakapofika mwaka 2025.

“Hatua hii ya kujiunga na VIRTUS ni moja ya juhudi ambazo sisi (TPSA)
tumechukua kwa ajili ya kukuza mchezo wa kuogelea hapa Tanzania na pia kuwapa nafasi watu wenye ulemavu wa akili kushiriki katika michezo na baadae waweze kushindana na wenzao hapa Tanzania na kwenye mashindano ya kimataifa,” amesema.

Advertisement

Katika hatua nyingine, TPSA wameteua makocha wawili wa Taifa ili waweze kusaidia program ya mazoezi ya wachezaji wenye ulemavu wa akili.

SOMA: Waogeleaji wanne kwenda Kenya leo

Makocha hao ni Julius Felix Maganga na Kocha Innocent Jonas watakaosaidiana na makocha wengine nane kuwaandaa wachezaji na kuwasaidia kufanya mazoezi katika mabwawa tofauti hapa Dar es Salaaam ili kusaidia kuimarisha viwango vyao.