BODI ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Bodi ya Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) wakutana kujadili namna bora ya kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa .
Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Angelina Ngalula katika kikao hicho amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vyama vya Biashara chini vinaratibiwa ipasavyo kwa ajili ya kuleta kuleta ufanisi.
“Nchini kuna zaidi ya vyama 2000 vya biashara vidogo na vikubwa na idadi hiyo inaendelea kukua.
Hii inaashiria kuwa Sekta Binafsi nchini inakuwa kwa kasi na ni muda muafaka kuwepo na usimamizi mzuri wa vyama hivi ili kuhakikisha vyama vinaendeshwa kwa ufanisi.
“Tunafahamu TCCIA imekasimia majukumu ya kuendesha mabaraza ya biashara ya mikoa na Wilaya. Lakini kama tulivyomsikia Rais, bado tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha mabaraza haya yanafanyika kwa wakati lakini pia wajumbe wa mabaraza wawe na sifa za kushahuri serikali kwenye ngazi zote,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Raisi wa TCCIA Edmund Mkwawa ameeleza juu ya umuhimu wa umoja wa sekta binafsi katika kuhakikisha inakua.
“Tusikubali kugawanyika kwa maslahi ya watu wachache, kama viongozi wa Sekta Binafsi tuna jukumu kubwa la kuhakikisha vyama vyetu vinahimarishwa na kufanya kazi kwa pamoja. Jukumu letu liwe kuhakikisha Sekta Binafsi ya Tanzania, inakuwa shindani yenye kuleta ajira, kipato na kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla wao”.
amesema.
TPSF na TCCIA wamedhamiria kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa manufaa mapana ya nchi.
Kikao hicho kimetokana na maelekezo aliyotoa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara Juni 9 mwaka huu mkoani Dar es Salaam.
Katija mkutano huo Rais Samia alielekeza Sekta Binafsi nchini kujitathmini ueendeshaji wake na kuhakikisha kuwa mabaraza ya biashara ya mikoa na Wilaya yanaimarika.
Comments are closed.