TRA yajivua Cask Bar kufungwa
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na kufungwa kwa The Cask Bar & Grill jijini Mwanza.
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Agosti 17, 2023 TRA imesema “Tunaomba wahusika na umma wawasiliane na mamlaka husika juu ya jambo hilo”.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Kiomono Kibamba jana alitangaza kufungwa kwa baa hiyo kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutokuwa na leseni ya biashara kwa miaka miwili.