TRA yataka ulipaji kodi kwa wakati

DSM; MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeziagiza taasisi za umma zenye madeni ya kodi kuhakikisha zinalipa ndani ya muda uliowekwa.

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ametoa agizo hilo alipokutana na taasisi hizo kwa ajili ya kuzijengea uwezo kuhusu ulipaji wa kodi.

“Taasisi zote za umma zinapaswa kulipa kodi kama jambo la lazima na sio hiari. Natambua taasisi hizi zipo katika makundi ya mashirika ya serikali yaliyoorodheshwa kupata faida na yale yasiyofanya biashara,” amesema.

Amehimiza kuwa katika taasisi za umma wajibu wa ulipaji kodi kwa makundi yote mawili hautofautiani.

“Mashirika ya umma yanaweza kuwa na uelewa zaidi kuliko taasisi myingine za umma ambazo hazipati faida.

” Naziomba taasisi zote za umma zinazohitaji uelewa wa kodi zihakikishe zinashirikiana nasi ili kupata uelewa zaidi. TRA imejipanga kushirikiana vizuri na taasisi zote za umma,” amesema.

Amesema TRA ilifanya maboresho ya muundo wa taasisi ulioanza kutumika Julai mosi mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button