TRA yatoa elimu ya mlipakodi kahama
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama imetoa elimu kwa watu wenye walemavu wa kutosikia (viziwi ) namna ya kuwa wazalendo katika ulipaji kodi.
Ofisa mawasiliano na elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka hiyo, Aniceth Ndailagije amesema hayo jana katika mafunzo ya siku moja kwenye Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kwa Wilaya ya Kahama inayojumuisha Halmashauri Msalala, Ushetu na Manispaa Kahama.
“Tunaomba elimu hii mmeipata mkatoe ushirikiano na muwe mabalozi wazuri kwa wengine kwa kuzifahamu sheria na kanuni zake ikiwa kila mwaka wa fedha serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeenda ikiziboresha zaidi na mzisome au kuomba ufafanuzi kwenye mamlaka husika.” amesema Ndailagije.
Ndailagije amesema kupitia kundi hili na chama chenu mnayo fursa ya kuiwezesha serikali kupata mapato yake stahiki na hatimaye kutoa huduma bora zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi.
Ndailagije amesema watii wajibu wa kulipa kodi kwani taifa lolote ikiwemo Tanzania linaendeshwa kwa shughuli za fedha zitokanazo na kodi zinazolipwa na wananchi wake.
Ndailagije amesema elimu iliyotolewa waizingatie kwani itawajengea uwezo wao wa kusikia kulipa kodi kwa wakati pamoja na kutatua changamoto zao wanazo kutananazo katika mazingira ya biashara.
Zawadi masoudi CHAVITA Wilaya ya Kahama amesema waliiomba mamlaka hiyo kuwapatia elimu ya mlipa kodi na TRA imewaona na kuwaletea mafunzo ili waifahamu sheria zilizopo.
“Tunaipongeza mamlaka hii tumejifunza vitu ambavyo hatukuvijua ikiwa baadhi yetu ni wafanyabiashara watakuwa wamenufaika.”amesema Zawadi.