SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imesema ukosefu wa nishati ya umeme katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam kwa siku chache zilizopita ni kutokana na ongezeko la matumizi kwa watu.
Kutokana na hilo, wameboresha miundombinu ikiwemo ufingaji wa transfoma mbili za MVA 175 katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi ili kuboresha upatikanaji wa umeme nchini.
Akizungumza leo alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha kinyerezi 1 Naibu Waziri wa Nishati, Judithi kapinga amesema kwa sasa jiji hilo limekuwa na matumizi makubwa ya umeme kutoka asilimia 6 hadi 16 hali iliyoifanya serikali kufanya uwekezaji wa transfoma zenye uwezo mkubwa.
Hata hivyo Kapinga amesema kwa sasa hali ya umeme inaridhisha huku akielezea maeneo ambayo yatanufiaka kutokana na uboreshaji wa miundombinu pamoja na transfoma ambapo maeneo ya kigamboni Mbagala pamoja na Mkuranga yatanufaika na hivyo kupunguza changamoto ya umeme mdogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanesco, mhandisi Gissima Nyamu -Hanga amesema transfoma hizo mbili zitafungwa kinyerezi na kufanya uwezo wa kituo hicho kufikisha mva 400 huku pia transfoma za mva 120 zikitarajiwa kufungwa mbagala na gongo la mboto na hivyo kujabiliana na ongezeko la matumizi ya umeme.