Treni ya Haraka kuanza safari za Dar – Moro

DAR ES SALAAM – SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari za treni ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro ambapo kuanzia Julai 5, abiria wataanza kutumia treni ya haraka (express train) isiyosimama vituo vya kati.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk leo Julai Mosi imesema TRC itaendelea kuongeza safari za kwenda na kutoka Dar es Salaam na Morogoro.

“Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asibuhi na 01:10 jioni na itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 01:30 usiku na treni ya kawaida itaondoka Dar es Salaam 03:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na kwa Morogoro itaondoka saa 03:50 asubuhi na 10:20 jioni.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

SOMA: Wakandarasi wanaochelewesha miradi ya maji kutolipwa

Nauli za SGR Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR (kawaida) zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari na umri wa abiria. Kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12, nauli ni Tsh. 69.51 kwa kila kilomita. Watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12 watalipa nusu ya bei hiyo, yaani Tsh. 34.76 kwa kilomita. Watoto chini ya miaka minne watasafiri bure, lakini taarifa zao zitahitajika kurekodiwa.

Nauli kwa Abiria Wenye Umri Zaidi ya Miaka 12

Daraja la Kawaida:

Safari Umbali (Km) Nauli (Shilingi)
Dar es Salaam – Pugu 19 1,000
Dar es Salaam – Soga 51 4,000
Dar es Salaam – Ruvu 73 5,000
Dar es Salaam – Ngerengere 134.5 9,000
Dar es Salaam – Morogoro 192 13,000
Dar es Salaam – Mkata 229 16,000
Dar es Salaam – Kilosa 265 18,000
Dar es Salaam – Kidete 312 22,000
Dar es Salaam – Gulwe 354.7 25,000
Dar es Salaam – Igandu 387.5 27,000
Dar es Salaam – Dodoma 444 31,000
Dar es Salaam – Bahi 501.6 35,000
Dar es Salaam – Makutupora 531 37,000

Nauli kwa Watoto Wenye Umri Kati ya Miaka 4 hadi 12

Daraja la Kawaida:

Safari Umbali (Km) Nauli (Shilingi)
Dar es Salaam – Pugu 19 500
Dar es Salaam – Soga 51 2,000
Dar es Salaam – Ruvu 73 2,500
Dar es Salaam – Ngerengere 134.5 4,500
Dar es Salaam – Morogoro 192 6,500
Dar es Salaam – Mkata 229 8,000
Dar es Salaam – Kilosa 265 9,000
Dar es Salaam – Kidete 312 11,000
Dar es Salaam – Gulwe 354.7 12,500
Dar es Salaam – Igandu 387.5 13,500
Dar es Salaam – Dodoma 444 15,500
Dar es Salaam – Bahi 501.6 17,500
Dar es Salaam – Makutupora 531 18,500

Masharti Kabla ya Safari Kuanza

LATRA imetoa masharti kadhaa ambayo yanapaswa kutimizwa kabla ya kuanza kwa safari za SGR. Masharti haya ni pamoja na:

  • Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa na leseni ya usafirishaji
  • Miundombinu ya reli na mabehewa kuwa na ithibati ya usalama
  • Matumizi ya mfumo wa utoaji tiketi za kielektroniki
  • Kuunganishwa kwa mfumo wa tiketi na mifumo ya LATRA
  • Uwepo wa watumishi waliothibitishwa na waliosajiliwa na LATRA

Habari Zifananazo

Back to top button