Trump: Ahadi ya Mabadiliko na Kumaliza Migogoro

MAREKANI: Rais wa zamani wa Marekani ambaye pia mgombea wa Urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican ,Donald Trump amesema angepunguza mfumuko wa bei, uhamiaji haramu na kukomesha vita endapo angekuwa madarakani.  

SOMA: https://www.aljazeera.com/news/2024/7/19/key-takeaways-from-trumps-speech-at-the-republican-national-convention

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa Chama cha Republican, Trump ameelezea nia yake ya kuboresha maisha ya Wamarekani. “Ni wakati wa mabadiliko,” alisisitiza Trump.

Advertisement

Trump amesisitiza heshima yake kwa wapigania uhuru ambao wameunda historia ya Marekani.

“Wapigania uhuru Wamarekani walijitokeza vitani, wakavamia ngome za maadui, na kusimama imara kwa ajili ya uhuru wetu,” alisema.

 SOMA: https://www.aljazeera.com/news/2024/7/19/key-takeaways-from-trumps-speech-at-the-republican-national-convention

Aliongeza, “Kama wazee wetu, sasa ni lazima tuungane, tuache tofauti zetu na mizozo ya zamani, na kusonga mbele kama taifa moja.”

Chama cha Republican kimeahidi kuendeleza sera zake za kusaidia Wamarekani waliosahaulika.,

“Kwa wale wote ambao mmepuuzwa kutelekezwa, na kuachwa nyuma, hamtasahaulika tena,” Trump alihitimisha.

Chanzo: BBC

/* */