MAREKANI : RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameikosoa ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kitaifa la Washington, akieleza kuwa haikuwa ya kuridhisha kwake.
Ibada hiyo iliongozwa na Askofu Mariann Edgar Budde, ambaye alimuomba Rais Trump kuwa na moyo wa huruma kwa wapenzi wa jinsia moja (LGBT) na wahamiaji haramu, akionyesha wasiwasi kuhusu hofu inayozidi kuongezeka miongoni mwa jamii hizi.
Muda mfupi baada ya kuapishwa rasmi, Trump alisisitiza kauli yake ya kwamba “kuna jinsia mbili tu” – ya kiume na ya kike, akifuatia kwa kusema kuwa ataendeleza juhudi za kukomesha uhamiaji haramu na kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji haramu walioko nchini Marekani. SOMA : Rais Trump kuapishwa leo
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ibada hiyo, Trump alisema: “Ibada haikuwa nzuri kwangu. Wanaweza kufanya vyema zaidi,” aliongeza kabla ya kuondoka.