Trump aongeza ushuru bidhaa za nje

WASHINGTON : RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru mpya kwa bidhaa mbalimbali zinazoagizwa kutoka nje, ikiwemo dawa na malori makubwa ya mizigo.
Ushuru huo unatarajiwa kupanda hadi asilimia 100 kwa baadhi ya dawa, huku malori makubwa yakitozwa ushuru wa asilimia 25 na vifaa vya jikoni na bafuni vikiongezwa ushuru wa asilimia 50. Hatua hiyo inalenga kulinda masoko ya ndani na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya Marekani. SOMA: BRICS yapingana na ushuru wa Trump
Kupitia ukurasa wake wa Truth Social, Rais Trump alisema bidhaa nyingi kutoka nje zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu kiasi cha kushusha thamani ya bidhaa za ndani. Hata hivyo, wafanyabiashara nchini humo wamepinga uamuzi huo na kuitaka Ikulu kusitisha ongezeko la ushuru.