MAREKANI : WIZARA ya Sheria nchini Marekani kwa kushirikiana na mwendesha mashtaka maalum,Jack Smith wako katika majadiliano kuhusu jinsi ya kumaliza mashtaka dhidi ya Donald Trump.
Smith kwa sasa anaongoza kesi nyingi dhidi ya Trump, ambaye atakuwa rais wa kwanza kuchukua madaraka wakati akikabiliwa na kesi kadhaa.
Hii ni pamoja na kesi ya madai ya matumizi mabaya ya nyaraka za siri, na ile inayohusu juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake kwa uchaguzi wa 2020 ambapo Joe Biden alishinda.
SOMA : Trump ashinda uchaguzi Marekani
Comments are closed.