TRUMP kutogombea tena urais

MAREKANI : RAIS wa zamani wa Marekani Donald Trump (78) amesema hatawania muhula wa nne mfululizo wa urais ikiwa atashindwa kwenye uchaguzi wa tarehe 5 Novemba Mwaka huu.

Ameyasema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa na Sinclair Media Group Septemba 23, nchini humo.

Trump aliulizwa ataweza kugombea tena katika miaka minne ijayo iwapo hatafanikiwa katika kuwania kiti cha urais kwa mara ya tatu mfululizo, rais huyo wa zamani alimwambia mwandishi wa habari wa Marekani Sharyl Attkisson: “Sidhani. Sidhani kwamba hilo litatokea. Sidhani kabisa. Tunatumai tutafanikiwa.”

Trump anakabiliwa na ushindani mkubwa dhidi ya mshindani wa chama cha Democrat Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, huku kura ya maoni ikionyesha ushindani mkali kati ya wagombea hao wawili katika majimbo ambayo yanaamua mshindi wa uchaguzi, licha ya kuwa Harris anaonekana kuongoza katika kura ya maoni kwenye ngazi ya taifa.

SOMATrump kagoma kutoshiriki mdahalo

Habari Zifananazo

Back to top button