TTF yatupilia mbali shauri la Feisal

KAMATI ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la soka TFF, limetupilia mbali shauri la mchezaji Feisal Salum na kwamba maombi yake ya marejeo hayana mashiko kisheria hivyo Feisal bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Taarifa iliyotolewa hivi punde na shirikisho la soka TFF imeeleza kuwa baada ya kukutana kwenye kikao leo na kusikiliza hoja za pande zote mbili kamati hiyo imeona shauri la Feisal halina msingi kisheria na haiwezi kubadili maamuzi ya awali.

Ikumbukwe Yanga ilipeleka shauri kwenye kamati hiyo ikimtaka Feisal kutoa maelezo kwanini ameondoka ndani ya kikosi hicho na kuandika barua ya kuaga akiichapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Disemba 24,2022 bila mazungumzo ya pande zote mbili.

Baada ya hapo shauri hilo kwa mara ya kwanza lilisikilizwa Ijumaa ya Januari 6 mwaka huu na baada ya hapo TFF ilitoa barua iliyoeleza Feisal bado ni mchezaji halali wa Yanga kimkataba na kutoa nafasi ya upande wa Feisal kuomba mapitio ‘Review’ ya shauri hilo kama hawataridhika na maamuzi yaliyotolewa.

Habari Zifananazo

Back to top button