Tume Maboresho ya Kodi yasheheni wabobezi kutimiza malengo

UUNDAJI wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni hatua muhimu na ya kimkakati kukabi li changamoto za kifedha nchini na kuchochea mabadiliko chanya ya kiuchumi.

Tume hiyo inajumuisha wata alamu wenye uzoefu kutoka sekta mbalimbali za kiutawala, taaluma, fedha, sheria na hata sekta binafsi.

Tume hii imeundwa kutoa njia mad hubuti ya marekebisho ya kodi.

Advertisement

Wasifu wa makamishna wa tume

Balozi Ombeni Yohana Sefue

Ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu na mwanadiplomasia nguli aliyebobea pia katika masuala ya utawala wa umma na sera.

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 47 katika utumishi wa umma na amehudumu kama Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mwakilishi Tanzania nchini Mexico.

Aidha, amehudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Canada na Mwakilishi Tanzania nchini Cuba, mwandishi wa hotuba na Msaidizi wa Rais wa Awamu ya Pili na ya Tatu.

Kwa miaka mitano alikuwa Mjumbe wa Jopo la Watu Mashuhuri wa Kutathimini Utawala Bora Barani Afrika (APRM). Pia, amekuwa mwenyekiti wa bodi na tume mbalimbali.

 

Profesa Florens D. Luoga

Ni Profesa Mshiriki mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mbobezi wa sheria za kodi, sheria za kiuchumi na biashara za kimataifa. Pia, ni Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania.

Amehudumu kama Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugen zi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania (GBT), Wakili Mwandamizi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa Tanzania na mshauri wa kisheria katika masuala mbalimbali katika utumishi wa umma.

 

Amehudumu katika utumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 37.

Profesa Mussa J. Assad

Ni Profesa Mshiriki wa Uhasibu na Ukaguzi na Makamu Mkuu wa Chuo Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro.

Prof. Mussa Assad

Amehu dumu kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mwenyekiti wa Bodi ya Waha sibu na Wakaguzi Tanzania.  Ana uzoefu wa utumishi wa umma na binafsi kwa zaidi ya miaka 36.

Maimuna K. Tarishi

Ni Katibu Mkuu mstaafu aliye bobea katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo. Mratibu wa Maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma.

Amehudumu kama Katibu Mkuu katika ofisi na wizara mbalimbali, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna.

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Ana uzoefu wa utumishi wa umma wa zaidi ya miaka 38.

Mwanaidi S. Maajar

Ni wakili wa masuala ya sheria na taratibu za biashara na uwekezaji. Ni mmoja wa waanzilishi wa Kampuni ya mawakili ya REX Attorneys.

Alikuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza na Marekani. Ni Mwenyekiti Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kampuni nyingine binafsi na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika sekta binafsi na ya umma.

Leonard C. Mususa

Ni Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bia Tanzania na kampuni nyingine binafsi zisizopungua tano. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 45 katika ushauri wa kodi, biashara na ukaguzi wa mahesabu.

Aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa PriceWaterhouseCoopers (PWC) Tanzania, moja ya kampuni nne kubwa za uhasibu na huduma za kitaaluma duniani.

David T. Tarimo

Ni mbobezi wa masuala ya kodi kwa zaidi ya miaka 45.

Amehudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC) Tanzania, moja ya kampuni nne kubwa za hasibu na huduma za kitaaluma duniani.

Ameshiriki kwa kiwango kikubwa kushauri kuhusu uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini.

Aidha, ni mlezi wa vipaji na ubunifu. Rished M. Bade Ni mtaalamu wa kodi aliyehu dumu serikalini kwa zaidi ya miaka 30 katika nafasi mbalimbali ikiwamo Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Kamishna Mkuu wa Mam laka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya Barclays.

Abubakar M. Abubakar

Ni Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi Mam laka ya Mapato Zanzibar (ZRA). Amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Chemba ya Biashara ya Zanzibar (ZNCC).

Aidha, ni mbobezi wa masuala ya kodi, ukaguzi wa hesabu na utawala wa fedha anayehudumu kama Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Zanzibar, mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 wa mifumo ya kodi, ukaguzi wa hesabu na utawala wa fedha akiwa amehudumu pia katika Benki Kuu ya Tanzania kama mkaguzi wa ndani.

Tume hii inawakilisha timu imara ya wataalamu wenye uwezo wa kipekee kukabiliana na changamoto nyingi za kodi nchini Tanzania.

Kutokana na kuwa na wataalamu wa fani na sekta mbalimbali katika maeneo ya utawala, mifumo ya kisheria, sera za uchumi na ushuru wa kampuni, tume hii inayo nafasi nzuri zaidi kutoa njia sahihi na zenye marekebisho yenye tija.

Ingawa wajumbe wanaweza kuwa wanatoka katika fani tofauti za utaalamu, nguvu zao kupitia ushirikiano na uelewa wa pamoja zinatarajiwa kutoa mapendekezo yatakayowezesha utekelezaji wenye tija.

Malengo ya tume

Malengo ya Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi ni pamoja na kuchambua sera na sheria za kodi na kubaini maeneo ya kuboresha, kubaini athari za viwango vya kodi katika sekta ya uchumi, kufanya mapitio ya mifumo na mbinu za ukusanyaji wa mapato ya kodi na ya siyo ya kodi pamoja na kuchambua usimamizi na utekelezaji wa sheria za kodi na kuchambua mapato ya siyo ya kodi na namna yanavyoathiri sekta za uzalishaji.

Mengine ni kubainisha chan gamoto zinazoathiri utendaji wa mamlaka zinazosimamia uku sanyaji wa kodi, ushuru, tozo na ada mbalimbali, kuchambua usimamizi wa mapato ya mamlaka za udhibiti na serikali za mitaa, kupokea na ku chambua maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau, kupata uzoefu kutoka kwenye nchi ningine kuhusu masuala ya kodi na kuandaa ripoti na mapendekezo jumuishi.

Hitimisho Kuundwa kwa tume hii kunadhi hirisha kujitoa kwa Tanzania katika uboreshaji wa mfumo wake wa kodi ili kukidhi mahitaji ya uchumi una okua sambamba na idadi ya watu inayoongezeka.

Rais Dk Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba,4.

Chini ya uongozi wa kimkakati wa Rais Samia pamoja na utaalamu wa tume hii katika maeneo mbalim bali, inayo nafasi kubwa na muhimu kuunda mfumo wa kodi unaofaa zaidi, wenye usawa na unaolenga ukuaji.

Malengo hayo yaliyowekwa wazi na muundo wa timu wenye usawa yanaonesha njia kamili za kushughulikia masuala muhimu kama upanuzi wa vyanzo vya kodi, kuboresha ufuatiliaji na kukuza mazingira yafaayo kwa biashara.

Ingawa changamoto zinaweza kujitokeza, bado nguvu za pamoja za tume na muunganiko wa utaal amu wa kiufundi, pamoja na utawa la na diplomasia zinatoa uhakika wa matokeo yanayoweza kutekelezeka na kuleta athari chanya.

Jitihada hizi si tu kwamba zinalenga kuimarisha nguvu za Tanzania kifedha, bali pia zinatoa mfano bora wa utawala jumuishi na bunifu wa kisasa unaofungua njia kwa mustakabali wa usawa na uchumi endelevu.