Tume ya madini kuboresha mfumo usimamizi leseni

TUME ya Madini imesema kuwa kutakuwa na maboresho ya mfumo wa utoaji usimamizi wa leseni za madini (Landfolio) yanayotarajiwa kuanza jumatano Oktoba 30,2024 hadi Oktoba 31,2024.

Taarifa hiyo imetolewa na Oktoba 28,2024 na Wizara ya Madini kupita Tume ya Madini na kusainiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwomo ikieleza kuwa matengenezo hayo yanatarajiwa kuanza jumatano Oktoba 30,2024 saa 1:00 hadi Oktoba 31, 2024 saa 3:00.

Taarifa imeeleza kuwa wakati wa maboresho mfumo wa zamani utazimwa ili kuwezesha mfumo ulioboreshwa kuanza kufanya kazi rasmi Oktoba 31,2024, hivyo tume imeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa watumiaji wa mfumo wakati huo wa marekebisho.

Advertisement

SOMA: Vifungashio kuboreshwa kudhibiti utoroshaji madini