Tume yaundwa kuchunguza uvunjaji wa nyumba Kigombe

TANGA: Uongozi wa Mkoa wa Tanga umeunda timu maalumu kwa ajili ya kufuatilia kwa kina tukio la ubomoaji wa nyumba 67 katika eneo la Kigombe,katika kijiji cha Msakangoto, kilichotokea Mei 22, 2026

Hatua hiyo imekuja kufuatia madai kuwa ubomoaji huo ulifanywa na dalali wa mahakama bila kufuata taratibu stahiki, ikiwemo kutoshirikisha Jeshi la Polisi, wala uongozi wa mkoa na wilaya husika.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Tanga Dk Batlida Buriani asema kuwa tukio hilo lilihusisha ubomoaji wa nyumba kadhaa, huku baadhi zikivunjwa zikiwa na wazee ndani yake na kuacha kaya zaidi ya 180 zikiwa hazina makazi jambo lililoibua taharuki na maswali mengi.

RC Batlda amesema kuwa timu ya Uchunguzi imepewa jukumu la kubaini sababu za Jeshi la Polisi halikushirikishwa pamoja na sababu zilizopelekea kutumika kwa utaratibu huo wa ubomoaji.

“Tunaomba tujue kwanini hawakushirikisha vyombo vya usalama na kwanini walitumia utaratibu huo. Tutabaini maandalizi gani yalifanyika kuhakikisha kuwa, pamoja na kuvunja pale, wale wananchi wanakwenda wapi,” amesema.

Hata hivyo amesema kuwa eneo lililolengwa lilikuwa na ukubwa wa ekari 37, likiwa na miti mingi na vichaka, na wananchi walikuwa wakiliishi eneo hilo tangu mwaka 1937.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button