Tumieni mitandao kwa manufaa – Mihayo

 

WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu nchini wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii  kuwasaidia katika  masomo yao.
Hayo yamesemwa leo na meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya  Ziwa Francis Mihayo wakati wa utoaji wa Elimu ya mitandao ya kijamii iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kampasi ya Mwanza.
‘’Uelewa wa elimu ya mitandao ya kijamii na sheria zake bado upo chini kwa wanafunzi wengi kutokana na wengi walikuwa hawatumia simu janja,kishikwambia na kompyuta mpakato wakiwa  Sekondari,’’ amesema Mihayo.
Mihayo amesema mamlaka yao ina  jukumu la kuimarisha elimu kwa umma,uelewa na kuzifahamu huduma zinazosimamiwa na TCRA.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino(SAUT) Profesa Balozi Costaricky Mahalu amewataka wanafunzi wa chuo hicho kutumia vyema mitandao ya kijamii na kuacha tabia ya kusambaza picha za utupu na jumbe za kichochezi katika mitandao hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button