‘Tutaifunga Yanga hadi niondoke Simba’

MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu

MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu amesema ahadi aliyotoa kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya kuifunga Yanga itaendelea kwa miaka minne mpaka atakapoondoka madarakani.

Akizungumza na HabariLEO, kiongozi huyo amesema watu wengi ikiwemo mashabiki wa Yanga, walimponda na kumbeza, lakini athari yake imeonekana jana baada ya kipigo cha mabao 2-0  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Wakati natoa ahadi ile sikuwa na bahatisha, nilikuwa na uhakika na timu yangu na Yanga wanatakiwa kujua kwamba pale siyo mwisho tutaendelea kuwafunga hadi niondoke madarakani, ndio ahadi inaisha,” amesema Mangungu.

Advertisement

Mangungu anatarajiwa kuiongoza Simba, hadi Januari 2026 kipindi ambacho uongozi wake utafika kikomo baada ya kufanyika kwa uchaguzi mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *