‘Tuwaombee viongozi tudumishe umoja’

MTWARA:MAKAMU wa Pili wa Raisi wa Zanzibar,  Hemedi Suleiman Abdullah amewaomba Watanzania kuwaombea viongozi wa serikali zote mbili ili kudumisha umoja, mshikamano wa kuimarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Abdullah pia amewataka viongozi, wazee na wengine wenye elimu ya muungano kuwaelimisha vijana kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili waendele kuenzi.

Abdulla ametoa rai hiyo leo Aprili 25, 2026  katika maadhimisho ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yamefanyika leo mkoani Mtwara.

“Niwaombe Watanzania wenzangu tuendelee kuwaunga mkono viongozi wa taifa letu, kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waendelee kudumisha amani na umoja wetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, Abdulla amesema tangu kuasisiwa kwa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, taifa limepata maendeleo makubwa pande zote mbili.

Ametaja Mkoa wa Mtwara serikali imefanya maendeleo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, na kilimo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button