SERIKALI imesema itahakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unakuwa jumuishi na shirikishi Ili kupata viongozi bora ambao watakaoweza kushirikiana katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani wakati wa mkutano wa uhamasisha wa wananchi kushiriki kwenye uandikishaji wa daftari la wapiga kura katika kata ya Kwediboma wilayani Kilindi.
Amesema kuwa mkoa huo imejipanga kushirikisha makundi yote kwa kuwapa utaratibu mzima wa shughuli zitakazofanyika kuelekea uchaguzi huo mwezi ujao.
“Tumejipanga kuhakikisha tunawapa taarifa makundi yote juu ya hatua zote za kuelekea uchaguzi huu kwani lengo ni kuhakikisha tunafanikisha uchaguzi huu Kwa kupata viongozi waliobora,”amesema RC Buriani.
Hata hivyo wananchi wa Wilaya ya Kilindi kuwa serikali imeweza kutoa hamasa kubwa ya wananchi kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kupiga kura hatua ambayo imesaidia kuleta msukumo mkubwa .
“Tumeweza kujitokeza Kwa wingi kwenye kujiandikisha hivyo kilio chetu ni tusaidiwe haki iweze kutendeka katika zoezi la uchukuaji wa fomu sambamba na kupata wagombea katika ngazi za vyama vya siasa “amesema Lazaro Semkwama.