Uchaguzi wazuia viongozi TOC kugombea Afrika

TANZANIA haina hata kiongozi mmoja katika uongozi mpya wa Chama Kikuu cha Olimpiki cha Afrika (ANOCA), ambacho kilifanya uchaguzi wake mkuu hivi karibuni.

Akizungumza Dar es Salaam juzi Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid alisema kuna wajumbe wa Tanzania walitaka kugombea Anoca, lakini kwa sababu TOC haijajafanya uchaguzi wake, hivyo wajumbe wake hawakuwa na sifa za kugombea.

Uchaguzi Mkuu wa Anoca ulifanyika hivi karibuni Algiers, Algeria na kupata viongozi wapya watakaokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne.

Advertisement

Gulam alisema katika mtandao wa Habari/Matukio, TOC kuwa wajumbe hao walishindwa pia, kuchaguliwa katika uchaguzi wa Kanda ya Tano ya Afrika kwa   kuwa walikosa uhalalili baada ya TOC kushindwa kufanya uchaguzi wake.

Uchaguzi Mkuu wa TOC ulipangwa kufanyika Desemba 28, mwaka jana jijini Dodoma lakini haukufanyika baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo nchini kuusimamisha.

Uongozi wa TOC unaendelea kuwepo madarakani hadi utakapofanyika tena uchaguzi wa kamati hiyo.

Marais wa kanda ndio wajumbe wa Anoca, ambapo Kanda ya Tano ilipo Tanzania walimchagua mwakilishi kutoka Uganda, Dk Donald Rukale, ambaye atawakilisha Kanda ya Tano katika Kamati Kuu ya Anoca.

Alisema kanda zingine nazo zilifanya uchaguzi wake, ampabo marais wa kanda ndio watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Anoca,

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *