UDSM yapata tuzo maonesho ufugaji, uvuvi

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeibuka kidedea katika maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuwa wa kwanza na kupata tuzo katika kundi la taasisi za elimu ya juu nchini.

Mkurugenzi wa Shahada za awali katika chuo hicho kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Dk Hezron Wanditi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea tuzo hiyo.

Dk Wanditi amesema ushindi huo umetokana na jinsi walivyojipanga kwa kuwa katika viwanja hivyo wa nane nane waliwasogezea huduma karibu wananchi na wadau mbalimbali wa elimu ambao walitaka kujiunga na chuo hicho.

Pia walikwenda na vitu mbalimbali pamoja na huduma ya udahili kwa wale wanaojiunga na shahada za kwanza na wale wanaojiunga na shahada za juu.

“Kuna baadhi ya wanafunzi wamepata huduma katika chuo chetu, pia tumekuja na miradi na bunifu mbalimbali zilizofanywa na chuo chetu,” amesema.

Amesema kwa pamoja vitu vyote walivyokwenda navyo vimewafanya kuwa washindi wa kwanza katika kundi la taasisi za elimu ya juu .

“Hii ni fahari kubwa sana kwetu kama UDSM. Hii imedhihirisha ni namna gani bado tuna mchango mkubwa kwa jamii na jamii inaamini tafiti zetu pamoja na ubunifu mbalimbali, yote hiyo inatoa faida kwa jamii,” amesema.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button