Ufafanuzi wa taarifa kuhusu kupotea kwa Gipson

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika mitandao na picha mjongeo ikimwonesha mwananchi aitwae Mercy Daniel Mkazi wa Arusha ambaye ameeleza kupotea kwa mume wake aitwae David Gipson Mkazi wa Arusha huku likiweka wazi kuwa Mtu huyo hashikiliwi na Jeshi hilo.

Akitoa taarifa hiyo leo Machi 18 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Jeshi hilo limepokea taarifa hiyo na uchunguzi wa shauri hilo unaendelea, katika ufuatiliji huku akibainisha kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa David Gipson amehusishwa na upotevu wa fedha uliotokea katika benki moja jijini Arusha(jina linahifadhiwa).

SACP Masejo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na ufuatiliaji wa shauri hilo ili kubaini mtu huyo yuko wapi na taarifa kamili itatolewa.

Ametoa wito kwa wananchi kusaidia Jeshi la Polisi kutoa taarifa za mtu huyo popote atakapoonekana. Pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili mkoa huo uendelee kuwa shwari.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Vavada to znane kasyno online, które działa również w Polsce. Strona przyciąga graczy szeroką ofertą gier, przejrzystymi warunkami i obsługą w PLN (zł). Bonus powitalny oraz intuicyjna obsługa sprawiają, że platforma zdobyła popularność wśród polskich użytkowników.

  2. Casino vavada zyskuje pozytywne opinie dzięki różnorodnej ofercie obejmującej sloty, gry stołowe oraz turnieje z evolution gaming. Kasyno online oferuje bonus powitalny, darmowe spiny i bonusy oraz kody promocyjne dla nowych graczy. Obsługa klienta gaming działa sprawnie, a gracze mogą wziąć udział w promocjach dostępnych na vavada pl.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button