Ufanisi wa taasisi washuka changamoto ukaguzi

DAR ES SALAAM: Chama Cha Wakaguzi wa Ndani (IIA Tanzania) kimesema miongoni mwa changamoto wanazokumbana katika ukaguzi ni viatarishi jambo linalopelekea kushuka kwa ufanisi katika taasisi wanapofanya ukaguzi.
Rais wa chama hicho, Jonathan Ngoma amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ufunguzi wa mwezi wa uhamasishaji wa ukaguzi wa ndani ambapo utadumu kwa mwezi huu mzima na kusema kuwa itakuwa ni kwa mikoa yote nchini.
Jonathani amesema miongoni mwa mambo wanayoyazingatia kwenye ukaguzi ni kuhakikisha viatarishi wanavizuia vyema ili kuweze kuwa na tija kwa taifa pamoja na jamii kwa ujumla.

“Sisi tunakuja kuangalia mpepewa ‘project’ hii sisi tunakuja kuangalia je mmefanya vitu vinavyotakiwa na miongozo inafatwa kwa hiyo kazi yetu kubwa ni kwenda kwa Bodi na kusema kwamba katika hizi project zizopangwa ni moja mbili Tatu vingapi vimefanyika vizuri kwa sababu tunaripoti vitu vizuri na vibaya ambavyo hujafika lakini tunatoa maoni.
‘Tunakaa pamoja Nini tuone turekebishe baada ya apo tunakaa na bodi tumeona hichi na tumekubaliana na management watafanya hivi hivyo watu wote tunategemeana katika utekelezaji majukumu,”amesema Jonathan.

Aidha, Jonathan amesema wanashauriana na taasisi waliyoifanyia ukaguzi lengo likiwa ni kuweza kufanikisha malengo waliyojiwekea huku kauli mbiu ya uhamasishaji wa ukaguzi wa ndani ni thamani ya ukaguzi wa ndani’




I’ve gained $17,240 only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, I was very troubled and thankfully I’ve located this project now in this way I’m in a position to receive thousand USD directly from home. Each individual certainly can do this easy work & make more greenbacks online by visiting
following website——>>> http://www.giftpay7.vip