Ufanisi Waongezwa Bandari ya Mtwara

MAMLAKA ya Bandari Mkoani Mtwara imesema mwaka huu inashirikiana na sekta binafsi kuendesha Bandari kavu kwa ajili ya kufungasha kontena za korosho ghafi zinazosafirishwa kupitia Bandari hiyo.

Meneja wa Bandari Ferdinand Nyathi amesema hayo leo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala  kukagua maeneo, shughuli na vifaa kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya korosho kupitia Bandari ya Mtwara kwa msimu wa korosho 2025/2026.

Nyathi amesema mpango wa kushirikiana na sekta binafsi  kupitia CFS (Container Freight Stations) za Bandari ni kuhakikisha ufanisi mkubwa katika kuhudumia  mzigo wa korosho.

Mkuu wa mkoa Kanali Patrick Sawala amesema  mkoa kwa kushirikiana na mamlaka ya Bandari umetenga eneo kwa ajili ya kufanyia  ‘staffing’ ya mizigo ya korosho. SOMA: Korosho Marathon 2025 yaiva

Amesema lengo ni kuhakikisha ufanisi mkubwa kuwawezesha wafanyabiashara na wasafirishaji kusafirisha mizigo yao kwa urahisi na kuendelea kutekelezwa agizo la serikali la kusafirisha korosho kupitia Bandari ya Mtwara.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button