Ufaransa yaitambua Palestina

PARIS: RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ametangaza kuwa nchi yake itaitambua rasmi Palestina kama taifa huru ifikapo Septemba mwaka huu, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Hatua hiyo inaiweka Ufaransa kuwa taifa lenye ushawishi mkubwa barani Ulaya kuchukua msimamo wa wazi kuhusu mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina.

Macron amesema ni muhimu kumaliza vita vinavyoendelea Gaza, kulinda ustawi wa raia na kuhakikisha taifa la Palestina linakuwa na uwezo wa kustawi kwa amani. SOMA: Ufaransa yajibu kitisho cha Algeria

Tangazo hilo limepokelewa kwa hasira na Israel, ambapo Naibu Waziri Mkuu, Yariv Levin, amelieleza uamuzi huo kuwa ni kuhalalisha vitendo vya kigaidi. “Ni aibu kuona Ufaransa ikiunga mkono Wapalestina,” alisema Levin.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema Marekani inapinga mpango huo, akidai Ufaransa imekurupuka katika uamuzi wake.

Chanzo: DW

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button