Ufaransa yajibu kitisho cha Ufaransa

ALGERIA : SERIKALI ya Ufaransa imetangaza kuwa itajibu hatua yoyote itakayochukuliwa na Algeria ya kuwafukuza wanadiplomasia wake 12, katika mzozo mpya wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Algeria imeeleza kutishia kuwafukuza wanadiplomasia hao ifikapo ndani ya saa 48, kufuatia malalamiko yake dhidi ya Ufaransa kwa kumweka kizuizini afisa wake wa ubalozi anayeshukiwa kuhusika katika utekaji nyara wa raia wa Algeria, mwishoni mwa wiki.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti kuwa wanadiplomasia hao wanachunguzwa pamoja na mtu mwingine kuhusu kutekwa kwa mpinzani wa Serikali ya Algeria, Amir Boukhors.

Advertisement

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, ameonya kuwa nchi yake itachukua hatua stahiki ikiwa kitisho cha Algeria kitatekelezwa.

Mahusiano kati ya Paris na Algiers yamekuwa ya kukatika tangu mwaka jana, wakati Rais Emmanuel Macron alipoikosoa Algeria akiiunga mkono Morocco katika mgogoro wa Sahara Magharibi.

SOMA : Marekani Ufaransa kuijadili mashariki ya kati

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *