UFARANSA: WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani anayemaliza muda wake Antony Blinken ameanza ziara ya kikazi nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la habari la AFP limesema kuwa lengo la ziara ni kutafuta ushirikiano kuhusu eneo lenye misukosuko la Mashariki ya Kati.
Katika ziara hii,Blinken atakutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye atamkabidhi nishani ya heshima ya juu zaidi ya Ufaransa.
Pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot kwa mazungumzo yanayoangazia Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na Syria.