Blinken ataka amani Mashariki ya Kati
MISRI : Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken yuko mjini Cairo nchini Misri kutafuta makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas ambayo sasa yanazidi kuwa magumu kufuatia wimbi la mashambulizi yanayoendelea huko Lebanon.
Hii itakuwa ziara yake ya kumi huko Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita vya Gaza, Blinken atajadili hatua kadhaa zilizofanyika za upatanishi na maafisa wa Misri.
SOMA : Shambulizi Israel laua waru 40
Katika ziara yake, Blinken amepanga kukutana na Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi na baadaye kufanya mkutano wa pamoja na vyombo vya habari.
Hatahivyo Maafisa wa Marekani wamesema hawatarajii kuona makubwa katika ziara hiyo bali wanategemea kuweka shinikizo kwa pande mbili hizo ili waweze kusitisha mapigano.