Shambulizi Israel laua waru 40

ISRAEL : WATU 40 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la Israel kwenye kambi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao kutokana na vita huko Gaza.

Maafisa wa Palestina wamethibitisha idadi ya vifo hivyo. Israel imeeleza kuwa ilikuwa inawalenga wanamgambo wa Hamas.

Israel ilitenga eneo hilo kuwa eneo la kibinadamu kwa maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi kutokana na vita vya Israel na Hamas.

Israel inadai kuwa inajizuia kuwadhuru raia wakati wa mashambulizi yake na kuwatuhumu Hamas kwa vifo vya raia kutokana na mara nyingi kuendesha harakati zake katika maeneo ya makazi.

SOMA :  Marekani yasitisha msaada wa silaha Israel

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button