Ufaransa yapigwa tena wahuni washambulia faiba

 UFARANSA – Ufaransa imekumbwa na duru mpya ya vitendo vya hujuma, wakati huu shambulizi likilenga waendeshaji mawasiliano, polisi imesema.

Mitandao ya fiber optic ya waendeshaji kadhaa “iliharibiwa” katika maeneo sita ya Ufaransa, kulingana na taarifa ya polisi. Mji mkuu wa Paris, ambao kwa sasa ni mwenyeji wa michezo ya Olimpiki, haukuathirika.

Ufungaji wa kampuni za mawasiliano za Ufaransa za SFR na Bouygues Telecom ziliharibiwa, gazeti la Ufaransa la Le Parisien na BFM TV liliripoti. Kebo hizo zilikuwa zimekatwa kusini mwa Ufaransa, huku mitambo karibu na Luxembourg na Paris ikiharibiwa.

Advertisement

SOMA: TCRA yatoa WiFi ya dezo msibani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anayeshughulikia Masuala ya Kidijitali Marina Ferrari alithibitisha vitendo vya uharibifu vilivyotekelezwa Jumapili usiku.