UFAWAZA wampa kongole Mavunde

UMOJA wa familia ya  wanamichezo wa zamani Dodoma(UFAWAZA) wametoa shukrani zao kwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwa udhamini wa Huduma ya Bima ya ‘NISHIKE MKONO’  inayotolewa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Akitoa salamu hizo Mwenyekiti wa  UFAWAZA, Ally  Kheri amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwa karibu na kuusaidia umoja huo tangu kuanzishwa kwake Novemba 27, 2021 ikiwa ni pamoja na udhamini wa bima ambao umegharimu  Sh milioni 3.6  kwa wanachama 75 .

Bima ya Nishike Mkono mwanachama ambae anapata tatizo la kufiwa upatiwa kiasi cha sh milioni 1.2

Akipokea shukrani hizo, Mavunde ameshukuru UFAWAZA kwa kutambua mchango wake na kuahidi kuendelea kushirikiano nao katika kuinua michezo Jijini Dodoma.

“Ninawashukuru kwa kutambua mchango wangu kwenye umoja wenu huu na nitaendelea kuwa nanyi bega kwa bega; ….. “Dodoma tumejipanga vizuri kuwapa heshima na kutambua mchango wa wanamichezo wa zamani.”Amesema

Mavunde, amesema, pamoja na  Bima hiyo  ya NISHIKE MKONO, hatua inayofuata ni kuhakikisha wanapata  uhakika wa Bima ya Afya ambapo kwa mujibu wa taratibu lazima wafikieshe idadi ya wanachama 100 ndio waingie  kwenye mfuko wa Umoja Afya  wa Bima ya Taifa.

“Tukikamilisha takwa hilo la usajili nitawachangia Sh milioni 5 kwa ajili ya malipo ya mfuko wa Umoja  Afya.” Amesema Mavunde

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button