Uganda kuongeza mtambo wa umeme

UGANDA : Uganda inatafuta ufadhili wa ujenzi wa mitambo mitatu ya kuzalisha umeme wa nyongeza wa maji wa zaidi ya megawati 1,600, kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo.

Afisa wa Wizara ya Nishati nchini Uganda, Julius Namusaga, ametaja maeneo matatu muhimu yaliyoko kwenye Mto Nile, ambako mitambo hiyo Ayago itakuwa mikubwa ambayo itazalisha  megawati 840.

Miradi mingine inayolengwa  kujengwa ni mtambo wa Kiba utakaozalisha megawati 400 na Oriang, megawati 392, na kufanya uzalishaji kufikia megawati 3,678 sawa na asilimia 80 ya uzalishaji wa sasa.

Advertisement

SOMA‘Nusu ya umeme Uganda hautumiki’

Hivi sasa, karibu asilimia 85 ya umeme wa Uganda unazalishwa na vituo vya umeme wa maji, na uliosalia unazalishwa na mitambo ya joto na jua.