Uganda kuzindua awamu ya tatu ya utafiti wa mafuta

KAMPALA : UGANDA itazindua awamu ya tatu ya utoaji leseni ya utafiti wa mafuta katika mwaka wa fedha unaoanza Julai.

Akitoa taarifa hiyo mjini Kampala hapo jana Alhamisi Waziri wa Nishati na Madini, Ruth Nankabirwa amesema Uganda iligundua mafuta ghafi katika bonde la Albertine Graben, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini shughuli za uchimbaji zilicheleweshwa.

Mnamo Agosti, nchi hiyo ilitangaza kuwa wanajiolojia wa serikali walikuwa wakifanya tafiti za awali katika mabonde mawili mapya upande wa kaskazini na kaskazini mashariki.

Vilevile, Waziri Nankabirwa ametangaza kuwa wizara yake imempata mshindi wa zabuni ya kuendeleza mradi wa mafuta. SOMA: Kenya, Uganda watatua mvutano wa petroli

 

Habari Zifananazo

Back to top button