Ujenzi kituo cha tahadhari ya Tsunami chafikia 25%

MRADI wa ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kanda ya Mashariki unaojumuisha kituo cha kutoa tahadhari za Tsunami nchini umefikia asilimia ishirini na tano.

Mradi huo unaojengwa kwa sh billion 10 unatarajiwa kukamilika Julai 2024.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dk. Buruhani Nyenzi amekagua maendeleo ya mradi huo, uliopo Kanda ya Mashariki na Kituo cha kutoa tahadhari za TSUNAMI nchini, unaotekelezwa katika maeneo ya SIMU 2000, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara yake, Dk.

Nyenzi amesema, chini ya Serikali ya Awamu wa Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, TMA imekuwa wanufaika wakubwa katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ukiwemo mradi huo ambao utahusika moja kwa moja katika utoaji wa tahadhari za TSUNAMI nchini na hivyo kuongeza tija katika mipango ya nchi.

Aidha, Dk. Nyenzi amefurahishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea kutokana na hatua mbalimbali ambazo mkandarasi amezichukua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi muda wa ziada na kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha makubaliano ya kimkataba yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.

Dk. Nyenzi amesisitiza matumizi ya malighafi zenye ubora na kutoa fursa za ajira kwa wazawa katika mradi huo.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button