Ujifunzaji tengenezeshi sekondari kuchochea ubunifu

MFUMO wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za sekondari nchini unapaswa kujengwa katika misingi ya kuwa tengenezeshi ili kuchochea stadi za ubunifu.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Huduma cha VETA mkoani Tabora, Dk Zebedayo Kyomo amesema hayo kwenye kongamano la nane la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STICE), linaloendelea jijini Dar es Salaam.

Dk Kyomo amesema badala ya kukaririshwa kanuni na nadhari pasipo uhalisia, misingi yakuwa tengenezeshi itachochea stadi za ubunifu kwa wanafunzi.

Katika mada aliyowasilisha katika kongamano hilo iliyojulikana kama ‘Kujenga Ubunifu kwa Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi katika Shule za Sekondari kupitia mazingira tengenezeti ya ujifunzaji’ Dk Kyomo amependekeza maboresho.

Dk Kyomo katika maboresho hayo amependekeza kupitia upya mihtasari ya masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari ili kupanua malengo ya ujifunzaji tengenezeshi.

“Mazingira ya ujifunzaji tengenezeshi ndio yakayochochea vijana kujenga stadi za ubunifu, hivyo kuwa sehemu ya Mapinduzi ya Nne ya Uchumi,” amesema.

Amesema hali ya ujifunzaji wa masomo ya sayansi nchini hivi sasa kwa kiasi kikubwa ni ya kurejea nadharia, kanuni na misingi ya kisayansi, lakini haimjengei mwanafunzi ari ya kudadisi na kutafsiri katika uhalisia.

Kongamano na Maonesho hayo (STICE) yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yakiwa na Kauli mbiu, “Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Shindani” na yanafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 14 hadi 16 Juni 2023.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button