Ukanda wa Nyasa mbioni kufaidi umeme REA

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) inakamilisha mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya ukanda wa Nyasa, baadhi vikiwa ndani ya Ziwa Nyasa. Vitongoji hivyo viko Ludewa, mkoani Njombe, na vingine Kyela, mkoani Mbeya, ambavyo ndani ya mwezi ujao vitafaidika na umeme wa uhakika.

Msimamizi wa Miradi wa REA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Danstan Kalugira, amesema vitongoji sita vitakavyofaidika ni Kitewele na Kimata (Ludewa) na Kiguru, Chanjale, Lumbuta na Nkanda (Kyela). Mradi ulianza Julai 13 mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Aprili 13 mwaka huu.

Kalugira alisema mradi unatekelezwa na mkandarasi SUMA JKT kwa gharama ya Sh. bilioni 3.1, huku kazi iliyobaki ikiwa ni kutandaza waya za umeme. Umeme unasafirishwa katika kilovoti 33 kutoka Kijiji cha Madunda, Kata ya Mawengi, hadi vitongoji husika. SOMA: REA kupeleka umeme vitongozi 474 Kagera

Msimamizi wa Mradi wa SUMA JKT, Yassin Selemani, amesema changamoto kubwa ni miundombinu ya barabara, mvua na milima, jambo linalolazimisha kusimika nguzo moja kwa siku. Hadi sasa nguzo 105 zimeshafungwa na sasa wanangojea kutandazwa kwa nyaya.

Kalugira pia alisema vijiji vyote 381 vya Mkoa wa Njombe vina umeme, huku kati ya vitongoji 1,833 vya mkoa huo, 1,249 vimeshafikiwa na umeme na 584 bado vimesalia. REA Nyanda za Juu Kusini inahudumia mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Ruvuma.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button