“Ukikataa ujauzito unarudi kwa mwanaume”

SUMBAWANGA: Chifu wa kabila la Wafipa, Mwene Kapufi III amesema kwa sasa adhabu anayopewa mwanaume akipatikana na hatia ya kumpatia msichana mwenye umri chini ya miaka 18 ni miaka 30 jela lakini kwao haikuwa hivyo katika mahakama ya watawala wa jadi wa kabila la Wafipa.
Mwene Kapufi III ambaye jina lake kamili ni Mwene Antony Thadeo Wangabo amesema adhabu iliyotolewa kwa mwanaume aliyempatia msichana na kukana kuwa hahusiki na ujauzito huo akitiwa hatiani na mahakama ya jadi ya kabila la Wafipa ilikuwa ujauzito wa msichana unahamishwa kwa wanaume huyo mpaka atakapokubali.
” Mahakamani iliwekwa sanamu ya mtoto wa kike akiwa mjamzito iliyofinyangwa kwa udogo wa mfinyanzi sasa mwanaume aliyetiwa hatiani kwa kumpatia msichana ujauzito halafu akaukana ujauzito huo basi aliamriwa kuigusa kwa mikono sanamu hiyo na mara moja ujauzito ulihamia kwake hadi atakapokubali,” amesema.
Mwene Kapufi ambaye ni mjukuu wa Mwene Ngalu,Chisi cha Mfipa ( Mwenye nchi ya Ufipa alibaisha hayo katika mahojiano maalumu na Habarileo Digital yaliyofanyika leo katika Jumba la Mwene lililopo eneo la Sumbawanga wenyeji katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mwene Ngalu ambaye ni mwanamke ndio muasisi wa jina la Sumbawanga ambao sasa ni Makao Makuu ya Mkoa wa Rukwa.Mwene Kapufi III ambaye ni mjukuu wake alitawazwa kuwa chifu Aprili 24, 2024.
Simulizi inayofuata ni maana ya jina Sumbawanga.