Ukioa,ukimpa mimba mwanafunzi,

Miaka 30 jela jumlisha umri wako, utazeeka - Majaliwa

WAZIRI  Mkuu Kassim Majaliwa amewata vijana na watu wengine kuepuka tabia ya kuwaoa au kuwapa mimba wanafunzi wa kike nchini.

Amesema kijana yoyote atakayekutwa ameao au kumtia mimba mwanafunzi wa shule yuko hatarini.

“Vijana nataka niwaambie mnanisikia na mnaniona ni marufuku kwenda kumshawishi mtoto wa shule kumuoa, ukikutwa umemuoa mwanafunzi wa shule, binti akakatiza masomo yake upo hatarini,” amesema Majaliwa.

Amesema kabla kijana yoyote hajaamua kufanya lolote na mwanafunzi wa ajiulize ana miaka mingapi.

“Sheria inayomlinda mtoto wa kike ni kali sana, kifungo chake ukikutwa ni miaka 30 jumlisha na umri wako, utarudi hapa umezeeka na hatutakujua usoni,” amesema.

Amesema,  Raisi Dk Samia Suluhu Hassan anataka kuona kila mtoto wa kitanzania anakwenda shule na anapata elimu na kwamba ametoa msisititizo watoto wote wa kiume na kike wasome.

 

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button