Ulega aipa tano Asas

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amefurahishwa na shughuli zinazofanywa na kampuni ya ASAS pamoja na wafugaji wote na wavuvi walioshiriki katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi.

Ulege ameonyesha furaha hiyo alipotembelea katika banda hilo la ASAS katika maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Amefurahia kuona ngamia wa maziwa, nyati wa maziwa, mbuzi wa maziwa na ng’ombe wa maziwa lakini pia kondoo wa kibiashara pamoja ng’ombe wa kufuga kwa ajili ya nyama.

Kwa upande mwingine, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Afri Farm Nyanda za Juu Kusini, Lipita Mtimila ameelezea mashine za kisasa za kukamulia ng’ombe ambazo zimebuniwa ili kurahisisha huduma hiyo kwa wafugaji wanaofuga kibiashara ambapo ng’ombe hukamuliwa kwa dakika tano hadi saba.

Amesema ufugaji wa kibiashara unahitaji uwekezaji kwenye teknolojia ya kisasa kwa kuwa mfugaji anapokuwa na ng’ombe wanaotoa lita 50 au 100 hawezi kukamua kwa mkono.

Amesema kampuni hiyo ina mashine mbalimbali za kukamulia ikiwa ni pamoja na mashine za kukamua ng’ombe wawili kwa pamoja.

Katika hatua nyingine amesema kama serikali inavyohamasisha wafugaji kutumia hereni ili kutambua mifugo yao, kampuni hiyo pia ina herein hizo za kisasa zitakazomwezesha mfugaji kutambua ng’ombe wake.

Habari Zifananazo

Back to top button