Ulinzi, usalama bandarini kusimamiwa na serikali

Tofauti na inavyosemwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na uwekezaji utakaofanyika bandarini, suala la ulinzi litabaki mikononi mwa Serikali.
Amesema “jukumu la Ulinzi na Usalama katika Bandari ya Dar es Salaam litaendela kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama”