Ummy aagiza huduma tiba kemia hospitali za rufaa za mikoa

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali zote za mikoa za Rufaa kuhakikisha zinatoa tiba kemia lengo ni kuwapunguzia wagonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo Dar es Salam.

Kiongozi huyo ametoa maagizo hayo leo akiwa jijini Arusha mara baada ya kutembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kuzindua maabara ya kisasa ya hospitali hiyo.

Waziri Ummy amesema tiba kemia hutolewa katika Hospital ya Rufaa ya  Muhimbili na Ocean Road tu na wagonjwa wamekuwa wengi hivyo ni wakati wa hospital za rufaa za mikoa kutoa huduma hiyo.

Ameusifu uongozi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru chini ya Mganga Mfawidhi Dk Alex Ernest kwa usafi, utoaji wa huduma safi na uwepo wa dawa na vifaa tiba na utendaji kazi na usimamizi wa dhati kwa watumishi na kutoa huduma kwa wananchi na kusema kuwa hospitali nyingine zinapaswa kuiga mfano huo.

Alisema Dk Alex ni mfano wa madaktari bingwa nchini kwani yuko karibu na watumishi wote wa hospitali hiyo na anatatua changamotozao zote hivyo madaktari wengine wa hospitali za rufaa wanapaswa kuiga mfano.

‘’Nimeridhishwa na usafi na utoaji huduma katika Hospitali hii ya Mount Meru kwani nimejionea mwenyewe na mnastahili pongezi na msibweteke hakikisheni mnaongeza kasi kwa maslahi ya wananchi’’alisema Mwalimu,”

”Rais Dk Samia Suluhu Hassan hatudai kwani emashafanya kazi yake ya kutoa fedha katika huduma ya Afya mamilioni ya fedha kote nchini hivyo ni wajibu wetu kutoa huduma safi kwa wananch.” alisema Ummy.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Charles Mkombachepa alimweleza waziri huyo kuwa Mkoa wa Arusha kwa sasa una vituo vya afya 431 hadi Desemba mwaka huu na serikali inamiliki vituo 259 sawa na asilimia 60 ukilinganisha na mwaka 2021/22 ambapo kulikuwa na vituo 241 sawa na asilimia 57 na taasisi za dini na binafsi zinamiliki vituo vya afya 172 sawa na asilimia 39.

Dk Mkombachepa alisema kuwa kuna hatua kubwa sana imepigwa katika kujenga na kuimarisha miundambinu ya kutolea huduma ya afya kwani katika 2021/22 kulikuwa na hospital 6 za halmashauri na kufikia Desemba mwaka huu halmashauri zote saba mkoani Arusha zina hospitali na zote zimeanza kutoa huduma.

Alisema mwak 2021/22 kulikuwa na vituo vya afya 37 na mwaka 2023/24 jumla ya vituo afya 3 vimeongezwa na kufikia 40,mwaka 2021/22 kulikuwa na zahanati 194 na mwaka 2023/24 zimeongezeka na kufikia zahanati 211,mwaka 2021/22 kulikuwa na vyumba vya upasuaji 17 ukilinganisha na mwaka 2023/24 kuna vyumba vya upasuaji 21 kwa vituo vya serikali.

Naye Mganga Mfawidhi Alex Ernest alimweleza Waziri Ummy kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru inanunuwa dawa MSD kwa fedha taslimu,wazabuni na wafanyakazi wa Hospital hiyo hawana deni nao kwa kuwa kila kitu wanachostahili kulipwa wameshalipwa au wanalipwa kwa wakati.

Dk Ernest alisema malewngo ya mkusanyo ya mwaka 2021/22 yalikuwa Sh bilioni 5 lakini hospitali hiyo ilivuka malengo na kukusanya zaidi ya Sh bilioni 6.

Alisema katika malengo ya makusanyo ya fedha katika kipindi cha julay mwaka 2023/24 hospitali hiyo imepanga malengo ya kukusanya Sh bilioni 7 lakini kwa kipindi cha miezi cha miezi sita hospital hiyo imeshakusanya zaidi ya Sh bilioni 4 na huenda malengo waliyokusudia watatimia na ikibidi kuyavuka bila ya kikwazo.

Habari Zifananazo

Back to top button