Ummy: Magonjwa ya ngono yameongezeka

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema magonjwa ya ngono yameongezeka nchini na kuitaka jamii hususani vijana kutumia kinga

Ummy, ameyasema hayo leo Mei 12,2023 bungeni mjini Dodoma akiwasilisha bajeti ya wizara yake.

“Kuna ongezeko kubwa la magonjwa ya ngono, idadi ya magonjwa ya ngono kwa mwaka jana ilikua¬† 458,612, sasa hivi imepanda na kufikia 480, 448, ” amesema na kuongeza:

“Nitoe¬† wito kwa Watanzania hasa vijana kutumia kinga, ili kujikinga na magonjwa ya ngono, ” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button