Wenza isiwe kikwazo kupata huduma – Waziri Ummy
TANGA; Muheza. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wauguzi wa afya kuwataka wajawazito kwenda na wenzao wao kliniki kwa ajili ya kupata huduma za afya
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 30, 2023, wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia lviwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.
Amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wajawazito kutakiwa kwenda na wenzao wao cliniki ndio watapewa huduma.
“Wapeni elimu juu ya umuhimu wa kujua afya ya mwenza wake na sio kumshinikiza, kwani huo ni sehemu ya ukatili, “amesema Waziri Ummy.